• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Ujenzi wa soko la kisasa Garissa wakaribia kukamilika

Ujenzi wa soko la kisasa Garissa wakaribia kukamilika

NA FARHIYA HUSSEIN

UJENZI wa soko la kisasa katika Kaunti ya Garissa umefikia asimimia 75, amesema Waziri wa Ardhi katika kaunti hiyo Abdi Omar.

Soko hilo litakua na wafanyabiashara zaidi ya 500 na wengine ambao kwa sasa wanafaendesha biashara zao katika soko la Orahey Open Air.

Kulingana na Bw Omar, soko hilo la kisasa inalenga kuhamishwa kwa  Soko la Orahey.

“Wafanyabiashara kwenye soko la Orahey watahamishwa.Soko la Orahey lilipangwa kuhamishwa kwa sababu ya changamoto ambazo wafanyabiashara wanazokabili kama vile vumbi, mvua, jua kali, mifugo na msongamano kando ya Barabara ya Posta, “alisema.

Akiongea wakati wa ukaguzi soko hilo, Bw Omar aliwahimiza wasiamizi kuharakisha kazi hiyo ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kama ilivyopangwa.

“Nyumba za serikali karibu na soko jipya zitabomolewa ili kuunda eneo la maegesho la wasaa kwa wafanyabiashara na wanunuzi,”Bw Omar alisema.

Waziri huyo pia alitembelea mradi wa mifereji ya maji na barabara kuu kando ya barabara ya Kismayu.

Alisema mradi huo uliopangwa kukamilika katika wiki tatu, utaboresha mfumo wa mifereji katika mji wa Garissa.

Aligundua kuwa mfumo duni wa mifereji ya maji umekuwa ukisababisha msiba katika mji wa Garissa wakati wa msimu wa mvua.

“Wafanyabiashara wengi na wamiliki wa nyumba wamepata hasara kubwa kwani maji ya mvua yalisababisha uharibifu na upotezaji wa bidhaa zilizopangwa na mafuriko makubwa,” alisema.

You can share this post!

Majina ya wanakamati bungeni kuidhinishwa Jumanne

Walimu, wanafunzi watoa kauli tofauti kuhusu KCPE

adminleo