• Nairobi
  • Last Updated March 19th, 2024 5:55 AM
Kesi ya mama aliyedai kuzaa na Maraga yatupwa

Kesi ya mama aliyedai kuzaa na Maraga yatupwa

Na Richard Munguti

MAHAKAMA ya kuamua kesi za watoto, Jumatano ilitupilia mbali kesi ambayo mwanamke alidai Jaji Mkuu David Maraga alitelekeza mtoto aliyezaa naye.

Mahakama ilisema kwamba mlalamishi, Mary Kwamboka, hakuzingatia kanuni za kuwasilisha kesi kwa sababu hakulipa ada ya Sh655 inayohitajika.

“Mlalamishi katika kesi hii, Mary Kwamboka, hakulipa ada inayotakiwa kulipwa kushtaki kesi kuhusu utunzaji wa mtoto au watoto,” mahakama hiyo ilisema ikitamatisha kesi dhidi ya Jaji Maraga.

Mary Kwamboka , mwanamke aliyedai alipata mtoto na Jaji Mkuu David Maraga. Picha/ Richard Munguti

Mawakili Danstan Omari na Anitah Masaki, waliomwakilisha Jaji Maraga, waliambia mahakama kwamba ushahidi wote uliotegemewa katika kesi hiyo ulikuwa feki.

Bw Omari alisema kesi hiyo ililenga kumharibia sifa Jaji Mkuu.

 

You can share this post!

DCI wafuata iwapo mtoto alitolewa kafara

Zimbabwe yarejesha kafyu

adminleo