• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 11:28 AM
Badi amuonya Sonko

Badi amuonya Sonko

Na COLLINS OMULO

Uhasama kati ya Gavana wa Nairobi Mike Sonko na Mkurugenzi wa Huduma ya Jiji la Nairobi na viunga vyake (NMS)

Mohammed Badi umeendelea kuchacha huku wakizozania nyumba rasmi la gavana mtaani Lavington. Mzozo huo mpya ulizuka Bw Sonko alipotangaza kwamba alitwaa nyumba hiyo iliyorejeshewa serikali ya kaunti na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC).

Alisema kwamba wafanyakazi wa serikali yake walikuwa wameanza kukarabati nyumba hiyo kabla yake kuanza kuishi ndani. Lakini baada ya tangazo hilo, Bw Badi alimuonya asiikaribie akisema iko mikononi mwa NMS.

“Masuala ya ardhi yalihamishiwa NMS na kwa hivyo nyumba hiyo ni mali ya NMS. Anaweza kutumia ujanja wake lakini tunapozungumza sasa hivi, tumeifunga na hakuna anayefaa kudai nyumba hiyo,” Bw Badi alisema.

BW Sonko naye alimjibu akimwambia aheshimu utawala wa sheria badala ya kutwaa nyumba hiyo kwa mabavu. Alidai Bw Badi pia alitwaa gari anayofaa kutumiwa wakati wa sherehe kama gavana wa Nairobi.

Alimtaka mkurugenzi huyo kutambua kwamba hawashindani mbali wanafaa kuelekeza juhudi zao kuwahudumia wakazi wa Nairobi.

“Ikiwa anataka vita, aende akapigane na magaidi wa Al Shabab huko Somalia. Hapa Nairobi, namuomba tuzingatie huduma kwa wakazi,” alisema.

You can share this post!

Mchuuza maji sasa amiliki chuo cha urembo

Arsenal yamuomba Auba kurefusha mkataba

adminleo