• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Mbunge ashtakiwa kwa kuuza gari kabla hajamaliza kulipa mkopo

Mbunge ashtakiwa kwa kuuza gari kabla hajamaliza kulipa mkopo

Na Benson Matheka na Stanley Ngotho

MBUNGE wa Kimilili Didmus Barasa Jumanne alishtakiwa kwa kuuza gari ambalo alikuwa amenunua kwa mkopo.

Bw Barasa ambaye ni mwandani wa Naibu Rais William Ruto alikamatwa baada ya benki ya Uwezo Microfinance kuripoti kwamba aliuza gari hilo kabla ya kukamilisha kulipa mkopo.

Kulingana na maelezo ya kesi, mbunge huyo alitenda kosa hilo 2017 mjini Kitengela, Kaunti ya Kajiado.

Katika mashtaka aliyokanusha mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kajiado Becky Cheloti yanasema kwamba, aliuza gari hilo aina ya Toyota Hiace kwa Sh450,000.

Kwenye shtaka tofauti ilidaiwa kwamba alipokea Sh450,000 kutoka kwa John Irungu akidai angemuuzia gari.

Mbunge huyo aliyewakilishwa na wakili John Khaminwa alikanusha mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh100,000.

Kesi hiyo itasikilizwa Novemba 27.Mnamo Julai 2020, alijaribu kuzuia kesi hiyo katika mahakama kuu lakini Jaji Luka Kimaru alitupilia mbali ombi lake na kuagiza ajibu mashtaka mbele ya mahakama ya Kajiado.

You can share this post!

Maseneta wakosa kuelewana kwa mara ya saba

Ujenzi wa daraja la watu pekee waanza Likoni

adminleo