• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 8:55 PM
Seneta Lelengwe aachiliwa huru bila masharti

Seneta Lelengwe aachiliwa huru bila masharti

Na CHARLES WASONGA

SENETA wa Samburu Steve Lelengwe mnamo Jumatatu, Agosti 17, usiku aliachiliwa huru baada kuhojiwa na maafisa wa upelelezi katika kituo cha polisi cha Maralala.

Lelegwe alikamatwa majira ya asubuhi katika eneo la Riverside alipokuwa wakielekea katika majengo ya Bunge kushiriki mjadala kuhusu mfumo wa ugavi wa fedha miongoni mwa kaunti.

Duru zinasema kuwa Bw Lelegwa alikamatwa kuhusiana na visa vya utovu wa usalama vilidaiwa kutekelezwa katika eneo la Baragoi mapema mwaka huu ambapo inadaiwa ngombe za wenyeji ziliibiwa.

Wakati huo huo mamia ya wakazi wakiwemo madiwani walifanya maandamano mjini Maralal usiku kulaani kukamatwa kwa Seneta Lelegwe.

Miongoni mwa waandamanaji walikuwa wahudumu wa bodaboda na makundi ya akina mama.

Diwani wa Wadi ya Ndoto Raisy Letura alishutumu serikali kwa kuwatisha maseneta ambao wanapinga mfumo wa ugavi wa fedha utakaopelekea kaunti 18 kupoteza kiasi kikubwa cha fedha ikilinganishwa na zile ambazo zilipokea katika mwaka wa kifedha wa 2019/2020.

“Hatuwezi kuvumilia vitisho kama hivi. Seneta Lelengwe ni kiongozi mwadilifu, hana rekodi ya uhalifu. Kwa hivyo, tunajua kuwa anatishwa kwa sababu serikali inataka kumlazimisha kuunga mkono mfumo utakaopelekea kaunti yetu kupoteza fedha,”akanukuliwa akisema.

Diwani Letura alisema wakazi wa Samburu wanamuuga mkono seneta waoa na wataendelea kufanya hivyo hadi siku ambayo “Samburu itapata haki yake.”

Kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti ya Samburu Christopher Lentukunye ni miongoni mwa wafuasi wa Seneta Lelengwe ambao walipiga kambi nje ya kituo cha polisi cha Maralal kulaani kukamatwa kwa kiongozi huyo.

You can share this post!

Inter yainyeshea Donetsk matano UEFA

Wizara yangu ilipokea Sh3b kati ya Sh48b – Kagwe