Cha kufanya ili usiwe na mafuta mengi tumboni
Na MARGARET MAINA
KUWA na mafuta mengi tumboni kuna athari za kiafya zinazoweza kusababisha mtu apate magonjwa mbalimbali kama vile shinikizo la damu na magonjwa mengineyo.
Hivyo ili kuepukana na athari hizo zitokanazo na mafuta tumboni unashauriwa kuzingatia mambo muhimu:
Chakula
Kula mboga za majani kwa wingi kwani husaidia sana kiafya.
Kunywa maji mengi sana.
Weka chakula cha kukutia hamu iliyopitiliza mbali na pahala ulipo.
Kula vyakula ambavyo vitatumika kwa kiwango kikubwa katika kujenga mwili wako ila epuka kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi.
Mazoezi ya viungo husaidia kupunguza tumbo kwa kiwango kikubwa.
Unaweza kufanya mazoezi ya aina nyingi ili kupunguza tumbo. Mazoezi yoyote ya nguvu yatapunguza mafuta ya mwili wako pamoja na mafuta ya ndani
Mazoezi ambayo nayazungumzia ni mazoezi ambayo yanasaidia kukata tumbo kwa kiwango cha juu sana. Mazoezi haya kwa karne hii ya teknolojia yapo wazi katika video mbalimbali.
Hivyo jaribu kutafuta video mbalimbali ambazo zitakusaidia kwa kiwango kikubwa katika kukata tumbo.
Hakikisha unapata usingizi wa kutosha kwa siku. Kupata usingizi kwa muda mzuri kuna mchango muhimu katika kudhibiti kiwango cha mafuta katika mwili wa binadamu.