Pabaya kwa kutumia barua feki ya ulemavu kuomba viza ya Amerika
Na BENSON MATHEKA
MWANAMUME alishtakiwa Jumanne kwa kutengeneza barua ghushi akidai iliandikwa na baraza la watu walio na ulemavu nchini na kuiwasilisha katika ubalozi wa Amerika kuomba viza.
Bw Jacob Katuyu Zakayo alikanusha kwamba alitaka kutumia barua hiyo kuomba viza kwenda Amerika kuhudhuria kongamano la watu wafupi.
Kulingana na shtaka, aliwasilisha barua hiyo Aprili 11 mwaka huu na kuambia maafisa wa ubalozi huo kwamba ilikuwa imeandikwa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Walemavu nchini, Bw Mohammed Gabbow.
Upande wa mashtaka kupitia polisi ulisema kwamba alishirikiana na watu wengine ambao hawakuwa kortini kutengeneza barua feki.
Barua hiyo inaonyesha yeye ni mwanachama wa chama cha watu walio na kimo kifupi nchini, Short Stature Society, na alikuwa amealikwa na chama cha Little People of Amerika kuhudhuria kongamano kati ya Julai 6 na 11 mwaka huu nchini Amerika.
Alishtakiwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Kibera Joyce Gandani na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh50,000 na mdhamini wa kiasi sawa au Sh30,000 pesa taslimu hadi Agosti 8 mwaka huu.
Na Benson Matheka
kesi itakapotajwa. Katika kesi tofauti, Bw John Lenyoiya alishtakiwa kwa kutengeneza barua feki akidai ilikuwa halali kutoka shirika lisilo la kiserikali la Maasai Youth Outreach (Mayoo) akitaka kuitumia kupata viza ya kwenda Amerika. Aliachiliwa pia kwa dhamana ya Sh50,000 na mdhamini wa kiasi sawa.