• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 8:50 AM
Kenya yaipa Japan msaada wa kilo 1,000 za majani chai

Kenya yaipa Japan msaada wa kilo 1,000 za majani chai

Na VALENTINE OBARA

KENYA imetoa msaada wa tani moja (kilo 1,000) ya majani chai kwa waathiriwa wa mafuriko ya maeneo ya magharibi mwa Japan, kwa mujibu wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni nchini.

Mafuriko yaliyotokea Japan wiki iliyopita yalisababisha vifo vya watu 219 huku idadi hiyo ikitarajiwa kupanda kwani shughuli za uokoaji zingali zinaendelea, na kuna watu karibu 20 ambao hawajulikani waliko.

Maelfu waliachwa bila makao baada ya mkasa huo ambao umesemekana kuwa janga baya zaidi la hali ya hewa kuwahi kuonekana kwa miongo mingi nchini humo.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni Kenya, Bi Monica Juma, alitoa ujumbe wa heri njema kwa niaba ya serikali na Wakenya alipokutana na Balozi wa Japan nchini, Bw Toshitsugu Uesawa afisini mwake Nairobi.

“Kwa niaba ya serikali na wananchi wa Kenya, ninatoa risala za rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika mkasa huu na kuwatakia waliojeruhiwa afueni ya haraka,” akasema waziri, kwenye taarifa iliyotumwa kwa vyumba vya habari.

Bi Juma aliongeza kuwa Kenya inathamini uhusiano wake na Japan kwani nchi hiyo imekuwa ikisaidia sana Kenya wakati wowote inapohitajika.

Mafuriko hayo yalifuatiwa na joto kali ambalo sasa limetishia kuathiri shughuli za kuokoa waathiriwa wa mafuriko, huku baadhi ya watu wakilazwa hospitalini kwa kuugua maradhi yanayosababishwa na joto jingi.

You can share this post!

HAKUNA KUPUMUA: Gharama ya maisha kuzidi kupanda

Mtalii ndani miaka 18 kwa kupapasa wasichana kutoka jamii...

adminleo