Mijeledi 80 kila mmoja kwa mashoga waliofumaniwa wakila 'uroda'
Na MASHIRIKA
ACEH, INDONESIA
WANAUME wawili walicharazwa viboko zaidi ya 80 baada ya kupatikana na hatia ya ushoga.
Ilisemekana wawili hao walihukumiwa katika Mahakama ya Kiislamu walipopatikana na hatia ya kufanya ngono.
Hukumu hiyo ya kuchapwa viboko ilitolewa mbele ya umati wa maelfu ya watu waliowakejeli.
Walikuwa wamekamatwa na kikundi cha watu ambao huchukizwa na ushoga ambao waliwawasilisha kwa polisi.
Kilichoshangaza ni kuwa kulikuwepo watalii katika umati huo waliokuwa wakipiga picha wawili hao wakicharazwa.
Nchini Indonesia, eneo hilo pekee ndilo hufuata sheria za Kiislamu na imekuwa kawaida kwa wahukumiwa kuadhibiwa hadharani sanasana kwa kuchapwa viboko au mijeledi.
Maafisa wa utawala huamini hatua hiyo huonyesha umma adhabu watakayopata ikiwa wataamua kukiuka sheria na kujihusisha na mienendo hiyo inayokiuka sheria za Kiislamu.
Mbali na ushoga, adhabu kama hiyo pia hutolewa kwa wanaouza au kutumia pombe, uchezaji Kamari au kushiriki ngono nje ya ndoa.
-Imekusanywa na Valentine Obara