Dondoo

Aduwaa wazazi wake kumtaka amsamehe mumewe mchepukaji

Na JANET KAVUNGA November 7th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

MWANADADA wa hapa aliomba wazazi wake wakome kuingilia ndoa yake walipomtaka amsamehe mumewe siku chache baada ya kumpata akirushana roho na wa pembeni.

Demu alikasirika na kurudi kwa wazazi wake na amekuwa na machungu kwa kuwa hakutarajia mumewe angeweza kuwa na mipango ya kando.

Juzi, wazazi wake walimtaka amsamehe mumewe na wakawa wanaongeza machungu moyoni mwake.

“Niliwaambia wakome kuingilia uhusiano wangu na mume wangu kwa kuwa alinikosea sana kwa kuchepuka ilhali nilimwamini sana. Sikutarajia wangenipa ushauri kama huo kwa sababu hata jamaa hakuonekana kujutia tabia yake,” demu alisema akisimulia masaibu yake kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii ambao vipusa hutumia kutapika nyongo.