Jombi atolewa jasho na mkewe kwa kumchafua kwa mpango wa kando
JAMAA wa hapa alijipata kona mbaya baada ya mkewe kupata jumbe anazotumiana na mpango wake wa kando.
Demu alilipuka kwa hasira alipogundua mumewe huwa anamsengenya na mpango wa kando. “Hii ni tabia gani unayoendeleza na mpango wako wa kando. Naona huwa unaniita mtu kisirani na kunitusi. Kwa hivyo huyu mpango wa kando ndiye wa maana? Utakiona cha mtema kuni,” mke wa jamaa alisema.
Jamaa alishtuka mkewe alikuwa akisoma arafa kwenye simu yake. Alijikunyata kama kuku aliyenyeshewa.
“Kama umenichoka niambie niende zangu badala ya kuniharibia jina,” demu aliwaka huku akifunganya virago vyake.