Dondoo

Kidosho ajigamba alivyozima mume ili aendelee kuchepuka

Na JANET KAVUNGA December 14th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

MWANADADA anayeishi hapa Shanzu jijini Mombasa alikemewa vikali na shoga zake kwa kujigamba jinsi alimsingizia mumewe makosa ili kuficha mienendo yake ya kuchepuka.

Jamaa aligundua mkewe hugawa tunda kwa polo mmoja na akaamua kumkabili akitishia kumfurusha nyumbani.

Hata hivyo demu alimwambia anafaa kujilaumu kwa kutowajibika vilivyo, na kudai ndiye sababu ya yeye kuchepuka.

“Nilimwambia ninachepuka kwa sababu hawajibiki. Hakuweza kukanusha kwani kazi yake humfunga hadi hana nafasi ya kutosha kula malavidavi nami. Jibu hilo lilimfyata ulimi na sasa naendelea kufurahia ngoma na mtu wangu,” mwanadada alisema na kuchachisha gumzo na wenzake ambao walimkemea vikali kwa tabia yake chwara.

Walimuonya kwamba michepuko yake itafika ukingoni na atajuta, huku wakimtaka atulie katika ndoa yake kwani ana bahati kuolewa na mume anayetia bidii kushughulikia familia yao.