Mdada afumania dume lake likichomoka kwa demu jirani
DEMU mmoja hakuamini alipofika hapa kumtembelea mumewe alfajiri na kushuhudia akitoka nyumba ya demu jirani katika ploti anayoishi.
Mkewe huyo alisafiri kutoka bara na akafika pwani alfajiri.
Alipata nyumba ya mumewe ikiwa imefungwa na akasubiri kwenye mlango akidhani alikuwa akifanya kazi zamu ya usiku.
Alipochelewa kufika, alimpigia simu, ikakiriza lakini haikuchukuliwa.
Baada ya dakika chache, mlango wa nyumba ya jirani ulifunguliwa na jamaa akachomoka nje akishika simu mkononi bila kutarajia kumpata mkewe.
Mwanadada hakuamini kwamba mumewe alikuwa akichepuka na jirani yake ambaye alimfahamu kwa miaka mingi. Jamaa alitokwa na kijasho huku mkewe akivumilia hasira zikimpanda, akamwitisha funguo za nyumba na akaingia ndani bila kuzusha.