Habari Mseto

KAWI YA JUA: KenGen yasaka ufadhili wa Sh5.7 bilioni

August 13th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na BERNARDINE MUTANU

Kampuni ya kuzalisha umeme (KenGen) inatafuta ufadhili wa Sh5.7 bilioni kufadhili ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha umeme kutokana na jua.

KenGen tayari imezungumza na wakopeshaji wa kimataifa ikiwemo ni pamoja na Benki Kuu ya Dunia, Benki ya French Development (AFD) na KfW, shirika la Ujerumani ambalo hufadhili miradi ya kampuni hiyo.

Ujenzi wa kiwanda cha uwezo wa megawati 45 unatarajiwa kuchukua miezi 14. Kiwanda hicho kitajengwa Embu karibu na Seven Forks Dam ambapo mradi huo utaitwa Seven Forks Solar.

Tayari uchunguzi kuhusu uwezo wa kufaulu kwa mradi huo umefanywa, alisema mkurugenzi wa maendeleo wa KenGen Moses Wekesa.

Mradi huo utazinduliwa katika kipande cha shamba cha hekta 100, Kaunti ya Embu.