• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Kushuka kwa bei ya Petroli kwawafaa wenye magari

Kushuka kwa bei ya Petroli kwawafaa wenye magari

Na BERNARDINE MUTANU

Kwa mara ya kwanza kwa muda mrefu bei ya mafuta nchini imeshuka. Ingawa sio kwa kiwango kikubwa, huenda kiwango hicho kikawafaidi sana waendeshaji magari.

Hii ni kutokana na kuwa bei ya Super Petrol ilishuka kwa shilingi 0.63 kutoka Sh107.46 Machi.

Pia, mafuta taa, ambayo hutumiwa na asilimia kubwa ya wananchi ilishuka kwa Sh0.73 hadi Sh76.72.

Hata hivyo, bei ya dizeli haikushuka, na itaendelea kuwa ilivyo kwa muda wa mwezi mmoja.

Mabadiliko hayo yalisababishwa na kushuka kwa viwango vya bei katika soko la kimataifa.

Tume ya Kudhibiti Kawi (ERC) mwezi jana lilipendekeza kuongezwa kwa bei ya mafuta ili kuwapa faida zaidi wauzaji wa mafuta.

Lilipendekeza kuongezwa kwa kiwango cha faida hadi Sh11.66 kwa lita ya mafuta kutoka Sh10.89 za sasa.

You can share this post!

ERC kuwakamata wanaouza mafuta yanayoharibu injini za magari

CBK yaonya Kenya itabanwa kuomba mikopo kimataifa

adminleo