Kutoa pesa ukitumia Paypal sasa utatozwa ada ya 1%
Na BERNARDINE MUTANU
Benki ya Equity imezindua ada mpya za malipo kwa wateja wa PayPal wanaotoa fedha kwa kutumia akaunti ya benki hiyo.
Kuanzia Machi mwaka huu, wateja watakuwa wakilipa hata kufikia asilimia moja kwa kutoa fedha kwa kutumia huduma hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Equity Dkt James Mwangi Jumatano alisema, “Kujumuishwa kwa wananchi wote katika huduma za kifedha kunaendelea kuwa kigezo kikuu katika mkakati wetu wa kibiashara.”
Kuchukua pesa kutoka PayPal hadi kwa akaunti ya Equity kutagharimu watumiaji wanaochukua dola zaidi ya 5001 asilimia moja pekee na wale wanaotoa kati ya dola kati ya 2001 hadi 5,000 watatoa kwa asilimia 1.125 ilhali watakaotoa fedha kati ya dola 1001 na 2000 itawagharimu asilimia 1.25. Watakaotoa kati ya 501 na 1000 watalipa asilimia 1.375 na watakatoa dola 500 au chini watalipa asilimia 1.5, alisema mkurugenzi huyo.
Huduma hiyo huwawezesha wateja wa Equity kukubali malipo kutoka popote ulimwenguni na kutolea pesa hizo nchini.
Kulingana na Dkt Mwangi, uzinduzi wa huduma hiyo itahakikisha kuwa watu wengi wamevutiwa kuitumia, “Tunatumai kuvutia matumizi zaidi ya huduma hiyo na miongoni mwa watumiaji wanaotumia PayPal,” alisema katika taarifa.