Habari Mseto

Mabwanyenye waongezeka kwa kasi nchini licha ya uchumi kuyumba

October 4th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na BERNARDINE MUTANU

LICHA ya kutatizika kiuchumi kwa sababu ya ukopaji kiholela na ufisadi serikalini, Kenya imeorodheshwa miongoni mwa mataifa 10 ulimwenguni ambayo yana mabwanyenye wanaokua haraka zaidi kihela.

Wakenya walio na thamani ya zaidi ya Sh3 bilioni waliongezeka kwa asilimia 11.7 mwaka 2017, mbele ya India, Hong Kong na Marekani.

Ripoti hii ni kwa mujibu wa Wealth X, shirika ambalo huchapisha ripoti ya kila mwaka kuhusiana na watu matajiri zaidi ulimwenguni.

Ingawa hakuna takwimu kamili ya idadi ya watu walioko katika kiwango hiki, katika muda wa miaka mitano, Kenya imeorodheshwa miongoni mwa mataifa yanayoendelea kukuza watu matajiri zaidi ulimwenguni.

Barani Afrika, kuna watu 2,490 walio matajiri kupindukia na ambao wanasimamia utajiri wa karibu Sh30 trilioni.

Kiwango cha kukua kwa matajiri hao kiliripotiwa kuwa asilimia 5.9.