Habari MsetoVideo

Motoni kwa kughushi 'payslip' kuonyesha anapokea mshahara wa mamilioni

June 13th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAUME alishtakiwa Jumtano kwa kujitengenezea stakabadhi ya malipo ya mshahara (payslip) kuonyesha anapokea kitita cha Sh2.7milioni kwa mwezi.

Bw Murage Kangi Murage alikanusha mashtaka zaidi ya 10 ya kupokea pesa kwa undanganyifu na kujifanya alikuwa anafanyia kazi shirika moja la kimataifa lijulikanalo kama Pathologist Lancet.

Bw Murage alikanusha mashtaka dhidi yake mbele ya hakimu mkuu katika mahakama ya Milimani Bw Francis Andayi.

Shtaka la kwanza dhidi ya mshtakiwa lilisema mnamo Machi 18 mwaka huu alipokea mkopo wa Sh40,000 kutoka kwa Bi Doreen Mututi akijifanya alikuwa ameajiriwa na kampuniĀ  ya Pathologist Lancet na kwamba alikuwa na uwezo wa kulipa deni hilo.

Bi Mututi alikuwa mkurugenzi wa kampuni hiyo ya kutoa huduma za fedha ijulikanayo kwa jina Double Link Investiments Limited.

Bw Murage alikabiliwa na shtaka la kujitengenezea cheti cha malipo ya mshahara kuonyesha alipata nyongeza ya mshahara kufikia Sh2,796,600 mnamo Aprili 9, 2018.

Mshukiwa huyo, upande wa mashtaka unaongozwa na Bw Solomon Naulikha ulisema haupingi mshtakiwa akiachiliwa kwa dhamana.

Mahakama ilimwachilia kwa dhamana ya Sh300,000 hadi Julai 18 kesi itakaposikizwa.

Video