• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 12:42 PM
Msichana aliyetembelea mpenziwe mtaani Umoja alivyoishia kunajisiwa kwa zamu

Msichana aliyetembelea mpenziwe mtaani Umoja alivyoishia kunajisiwa kwa zamu

NA JOSEPH NDUNDA

WANAUME wawili wanakodolea macho uwezekano wa kifungo cha maisha gerezani baada ya kushtakiwa kumnajisi msichana mmoja mwenye umri wa miaka 17 katika mtaa wa Umoja,Nairobi.

Wanaume hao, Kennedy Kangethe na Kelvin Kimani kwa jina lingine Salim wameshtakiwa kumnajisi kwa zamu msichana huyo aliyetambuliwa kwa herufi za jina JWL katika nyumba ya kukodisha ya Kangethe mnamo Desemba 21, 2023.

Wawili hao wameshtakiwa pia kwa kushiriki vitendo vya aibu na mtoto ambapo wote wawili wanashtakiwa kumgusa sehemu nyeti.

JWL alikuwa amemtembelea Kangethe, ambaye ni mpenziwe, na kumpata akiwa na Kimani.

Kangethe aliondoka kwenda kununua chakula na kumwacha mpenziwe na rafikiye wakiwa pamoja ndani ya nyumba.

Soma pia Mzee aliyeoa msichana wa miaka 16 ashtakiwa kwa unajisi

Halafu Mgeni aliye na mashtaka saba ya kunajisi watoto amjibu jaji akitabasamu bila kuonyesha majuto

Inadaiwa kwamba punde tu Kangethe alipoondoka, Kimani alianza kumsogelea msichana huyo akimtaka kufanya naye mapenzi.

Kimani anadaiwa kuchomoa kisu na kutishia kumdunga iwapo angepiga kelele au kujaribu kutoroka na hapo ndipo alimuamuru kuvua nguo na akafunga mlango.

Kangethe alirejea baadaye na kumpata rafikiye akimnajisi msichana na anadaiwa aliungana na rafikiye kuendelea kumnajisi kwa zamu.

JWL alitoroka wakati wawili hao walipoondoka nyumbani na akaenda hospitali ambapo alifanyiwa ukaguzi, akatibiwa na kushauriwa kupiga ripoti kwa kituo cha polisi.

Hakufahamisha wazazi wake kilichomtendekea. Wazazi wake waligundua kwamba alikuwa na sonona na wakajaribu kumuuliza kulikoni ila akasita kuwaeleza.

Msichana huyo baadaye Januari alifichua kwa mamake kilichofanyika na ndipo wakapiga ripoti kwa polisi.

Kangethe alitiwa mabroni baada ya kutambuliwa na msichana huyo.

Polisi wamebaini kwamba Kamau, ambaye ni mwanafunzi, tayari alikuwa kwenye rumande katika gereza la Viwandani baada ya kushtakiwa kwa kosa tofauti la wizi.

Wawili hao walikanusha mashtaka mbele ya Hakimu Mkuu Justus Kituku wa Makadara na kuomba wapewe dhamana nafuu kupitia wakili wao Mercy Mumbu.

Bi Mumbu aliambia mahakama kwamba Kangethe ni mwanafunzi katika chuo cha ufundi wa kiviwanda NITA na Kamau ni baba wa mtoto mchanga ambaye anamtegemea kimaisha.

Waliachiliwa kwa dhamana ya Sh300,000 au Sh200,000 pesa taslimu.

Kesi itaanza kusikizwa Juni 17, 2024.

  • Tags

You can share this post!

Kaunti nane kukosa umeme Kenya Power ikiboresha mfumo wake

Filamu ya Bobi Wine yapata uteuzi Oscars

T L