• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 5:55 AM
Mzee aliyeoa msichana wa miaka 16 ashtakiwa kwa unajisi

Mzee aliyeoa msichana wa miaka 16 ashtakiwa kwa unajisi

NA JOSEPH NDUNDA

MZEE wa miaka 50 aliyemuoa msichana wa miaka 16 anakabiliwa na mashtaka ya unajisi kinyume na kifungu cha 8 (1) (4) cha Sheria.

Caleb Oguma alishtakiwa kwa kumnajisi mtoto huyo tarehe tofauti kati ya Agosti 1 na Desemba 2, 2023 katika eneo la Darfur huko Kariobangi, Nairobi alikokuwa akiishi naye.

Anakabiliwa na shtaka lingine la kumnajisi msichana huyo kinyume na kifungu cha 11 (1) cha SOA ambapo anadaiwa kumshika mtoto huyo sehemu zake za siri kwa makusudi na isivyo halali katika kipindi hicho.

Mshukiwa huyo anayetoka Kaunti ya Migori alikutana na mtoto huyo na kumshawishi aandamane naye Nairobi baada ya kuahidi kuwa atampeleka kufanya kozi ya kushona nguo.

Alikuwa mwanafunzi wa Kidato cha Tatu.

Aliandamana naye hadi Nairobi baada ya kukubali ombi lake la kumsajili kwa kozi hiyo.

Hata hivyo, alipofika Nairobi, alimpeleka kwa mkewe na wakaendelea kuishi pamoja hadi afisa wa Nyumba Kumi alipogundua kuwa Oguma alikuwa ameoa msichana huyo.

Hata hivyo, Oguma alikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkuu Irene Gichobi wa Mahakama ya Makadara.

Mshukiwa huyo aliachiliwa kwa dhamana ya Sh200, 000 akisubiri kufikishwa mahakamani.

Kesi hiyo itatajwa Januari 10, 2024.


  • Tags

You can share this post!

Man U wafufuka, majirani zao Man City wakififia EPL

Wauzaji bangi wanavyotumia magari ya kifahari kuisafirisha

T L