BBI: NCIC yataka nguvu za kuwashtaki na kuwaadhibu wachochezi
Na WANDERI KAMAU
TUME ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) inataka ipewe nguvu za kuwashtaki na kuwaadhibu watu wanaopatikana kuwachochea wananchi.
Inataka nguvu hizo kulingana na zile za EACC na DPP.
Hili ni kupitia mwenyekiti wake Samuel Kobia ambaye amesema hayo wakati akitoa mapendekezo yake kwa Jopo la Mpango wa Maridhiano (BBI).