Obado aachiliwa kwa dhamana ya mamilioni
NA JOSEPH WANGUI
Gavana wa Migori Okoth Obado anayeshtakiwa kwa ufisadi ameachiliwa kwa dhamana ya Sh8.7 milioni ama pesa taslimu Sh2o milioni.
Jaji mkuu Lawrence Mugambi wa mahakama ya Milimani pia alitoa amri ya kumzuia Obado kutika afisini mwake.
Afisa anayechunguza kesi yake aliagizwa kumsindikiza Obado akachukue bidhaa zake kutoka afisini mwake.
Korti hiyo pia ilimzuia Obado kusafiri nje ya Kenya. Gavana Obado na wanawe ni washukiwa wa wizi ya mamilioni ya hela kutoka afisi za umma.
Alioshatakiwa nao waliachiliwa kwa dhamana ya kati ya Sh2 milioni na Sh8.2 milioni. Wote walizuiliwa kuingia afisi za kaunti.
TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA