SUKARI yote yenye nembo ya Mumias unayoinunua katika maduka ni feki. Ripoti hii ni kwa mujibu wa wabunge kutoka Magharibi mwa Kenya.
Wabunge hao watatu wamedai kuwa sukari ya magendo inapakiwa katika mifuko yenye nembo ya Mumias na kuuzwa kama sukari inayotoka kwa kampuni hiyo.
Wabunge hao, Godfrey Osotsi (maalum), Caleb Amisi (Saboti) na mwakilishi wa kike wa Busia Florence mutua walisema walaghai wa sukari wamebuni njama mpya ya kulemaza zaidi kampuni hiyo, ambayo haifanyi vyema kwa sasa.
Baada ya kupakiwa, sukari hiyo husambazwa kwa maduka ya rejareja kuuzwa maeneo mbali mbali nchini.
Zaidi, magunia yanamowekwa sukari hiyo hayana siku ya kutengenezwa au ya kuharibika.
Kwa muda wa miezi sita, kampuni ya Mumias haijatengeneza sukari.