Maajenti wa kimapokeo katika sekta ya utalii wanazidi kuumia kutokana na ujio wa teknolojia.
Wanapoteza hadi asilimia 60 ya soko kutokana na kuwa watalii sasa wanajihifadhia nafasi katika maeneo wanayotaka kutalii kwa kutumia mitandao na simu.
Kulingana na Chama cha Maajenti wa Usafiri (KATA) wamepoteza asilimia kubwa ya soko katika muda wa miaka 10 iliyopita.
Hiyo ni kumaanisha wanapoteza Sh39 milioni kila mwaka, kilisema chama hicho. Kwa sasa, watumiaji wa intaneti nchini ni milioni 36.09 kulingana na Tume ya Mawasiliano.
Hivyo, Wakenya wengi wanapata habari kuhusiana na sekta hiyo kwa mtandao, na hawahitaji tena mawakala kuwahifadhia mahoteli au hata ndege.
Mawakala hao sasa wameachiwa watu wanaosafiri kufanya biashara.