• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 10:55 AM
Tume kuhusu haki yaitaka serikali kutumia mbinu za kiutu Mau

Tume kuhusu haki yaitaka serikali kutumia mbinu za kiutu Mau

Na MAGDALENE WANJA

SERIKALI ya Kenya imeshtakiwa katika Tume ya Afrika kuhusu Haki za Kibinadamu na za Watu kwa kufurusha waliokuwa wanaishi katika msitu wa Mau kwa njia inayotajwa kuwa ni isiyofaa.

Akithibitisha hatua hiyo, wakili Duncan Ojwang alisema kuwa serikali ilikiuka sheria ilipokuwa ikiwafurusha watu kutoka msituni humo.

“Kilichoshuhudiwa ni ukiukaji mkubwa wa haki za kibinadamu hasa katika vipengee vya 3,5,14 na 17 vya African Charter,” akasema Bw Ojwang.

Bw Ojwang aliongeza kuwa lalama hizo ziliwasilishwa mnamo Septemba 30 katika baraza la Tume ya Afrika kuhusu Haki za Kibinadamu na za Watu.

Bw Ojwang ambaye pia ni mhadhiri wa maswala ya sheria katika chuo cha Arizona aliseam kuwa aliwasilisha lalama hiyo kwa ushirikiano na mashirika ya haki za kibinadamu hapa nchini.

Kando na lalama hizo, waliomba kuwa baraza hilo lisimamishe ufurushaji huo mara moja.

Uwezo

Alisema kuwa baada ya kusikiza lalama hizo, tume hiyo ina mamlaka ya kutatua kesi hiyo.

“Suala la msitu wa Mau ni la dharura na madhara ya ufurushaji huo yanaweza kuwa na athari kubwa,” akasema Bw Ojwang.

Tume hiyo inaitaka serikali kusimamisha hatua ya kuwafurusha watu kutoka kwa msitu huo mara moja.

Kufuatia lalama hizo, tume hiyo ilimuandikia barua Rais Uhuru Kenyatta ikimtaka kufuata amri hiyo.

You can share this post!

Jinsi mahakama ya Afrika inavyoshughulikia kesi zinazohusu...

Dow yashirikiana na ChildFund kuwapa watoto motisha...

adminleo