• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Uhuru kuachia Wakenya deni la Sh7 trilioni aking’atuka 2022

Uhuru kuachia Wakenya deni la Sh7 trilioni aking’atuka 2022

Na BERNARDINE MUTANU

DENI la Kenya litaongezeka hadi Sh 7 trilioni ifikapo 2022. Kufikia Juni mwaka 2019, deni hilo litagonga Sh5.6 trilioni.

Hii ni kulingana na ripoti ya kila mwaka kuhusu usimamizi wa madeni iliyotolewa na Waziri wa Fedha Henry Rotich, na iliyowasilishwa Bungeni Jumatano.

Ilionyesha kuwa kufikia Juni 2017, deni hilo lilikuwa ni Sh5.1 trilioni. Kati ya hizo Sh2.5 trilioni zilikuwa zimekopwa nchini ilhali Sh2.6 trilioni zilikuwa zimekopwa nje ya nchi.

Miongoni mwa wakopeshaji wakubwa ni China (Sh559.1 bilioni) Italia (Sh101.9 bilioni), Ujerumani (Sh34.7 bilioni), Ubelgiji (Sh10.2 bilioni) na Marekani (Sh2.9 bilioni).

Wengine ni International Development Association (IDA) – Sh516.8 bilioni, Africa Development Bank (ADB) – Sh204.8 bilioni na Benki ya Kimataifa ya Fedha(IMF) – Sh71.6 bilioni.

You can share this post!

NTSA kuwapa wenye magari vitabu vya kidijitali kuzima wizi

Wakenya watuma na kupokea Sh1 trilioni kwa simu kwa miezi 3

adminleo