• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:55 AM
Waahidi kuunga BBI

Waahidi kuunga BBI

Na WAANDISHI WETU

VIONGOZI kadhaa kutoka Pwani walitumia sherehe za Mashujaa Dei kupigia debe ripoti ya Mpango wa Maridhiano (BBI), inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.

Walisema wataiunga mkono ripoti hiyo ili kuleta fedha zaidi kwa kaunti.

Akihutubu Jumanne katika Shule ya Upili ya Mwatate, Gavana wa Taita Taveta, Bw Granton Samboja, alisema kuwa eneo hilo limeachwa nyuma kimaendeleo na ripoti hiyo itawafaidi wakazi kwa kuwapelekea fedha kufadhili miradi zaidi.

Ripoti inapendekeza mgao wa serikali za kaunti kuongezwa hadi asilimia 45 ya mapato ya jumla ya taifa.

“Ikiwa ripoti hiyo itapitishwa, tutapata huduma bora katika sekta za afya, maji, elimu, barabara kati ya zingine ambazo zimekwama kutokana na uhaba wa fedha,” akasema.

Gavana wa Kilifi, Bw Amason Kingi wa Kilifi, alisema kuwa BBI itasaidia kufanikisha mfumo wa ugatuzi.

You can share this post!

Serikali yasema Huduma Namba itaboresha maisha ya Wakenya

Wakenya kupokea kadi za Huduma Namba