Jaji Mkuu akemea kutekwa nyara kwa vijana wanaohusishwa na maandamano
JAJI Mkuu Martha Koome ameelezea wasiwasi wake kuhusu ripoti za kutekwa nyara kwa vijana wanaohusishwa na maandamano akisema huo ni ukiukaji mkubwa wa sheria na haki za kibinadamu.
Jaji Koome ametaka mashirika yote ya serikali yanayohusika na masuala ya haki kuheshimu majukumu ya kikatiba na kuhakikisha kwamba vitendo vyao vinaambatana na Katiba.
“Kukiuka haki kama zilivyonakiliwa kwenye sheria hakutaleta tu utovu wa usalama, kutavuruga utawala mzima wa kisheria kama unavyohitajika katika Kipengele cha 10 cha Katiba,” akasema.
Jaji Mkuu vilevile ameagiza majaji na mahakimu kujiandaa kuongeza muda wa kazi ili kushughulikia kesi zote za washukiwa wanaoletwa mbele ya mahakama na kushughulikia maombo yote ya kutaka aliyetekwa nyara kutolewa hadharani.