Waislamu kutoka Msikiti wa Nasjid Noor Mosque, Jijini Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu wakishiriki maadhimisho ya sikukuu ya Idd-Ul-Fitr kukamilisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, mnamo Jumatatu, Machi 31, 2025. PICHA|JARED NYATAYA
JAMII ya Waislamu kote ulimwenguni wamekamilisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, leo, Jumatatu, Machi 31, 2025 wakishiriki sherehe za Idd-Ul-Fitr.
Idd-Ul-Fitr, ni siku maalum iliyotengewa kusherehekewa mfungo wa mwezi mzima wa kusali.
Waislamu kutoka Msikiti wa Nasjid Noor Mosque, Jijini Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu wakishiriki maombi ya maadhimisho ya sikukuu ya Idd-Ul-Fitr kukamilisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, mnamo Jumatatu, Machi 31, 2025. PICHA|JARED NYATAYA
Mfungo huo, aidha, ulikamilika mnamo Jumapili, Machi 30, 2025.
Maeneo mbalimbali nchini, washirika wa jamii ya dini ya Kiislamu wamekongamana leo Jumatatu kwenye maeneo yao ya kuabudu – Msikiti kwa ibada ya maombi.