Kampuni 8 zilitumiwa kuchafulia Raila sifa 2013 na 2017
NA FAUSTINE NGILA
KAMPUNI nane zilitumiwa kumharibia sifa Kion- gozi wa ODM, Bw Raila Odinga mitandaoni wakati wa kampeni za chaguzi za 2013 na 2017, dhidi ya mpinzani wake Uhuru Kenyatta aliyewania kupitia Chama cha Jubilee, Taifa Leo imethibitisha.
Kampuni hizo zilituma jumbe zilizodai Bw Odinga anaabudu shetani, huku zingine zikidai kwamba ali- panga kumuua rais mstaafu, marehemu Daniel Moi ikiwa angeshinda urais.
Hata hivyo, jumbe hizo tayari zimefutwa kwenye intaneti. Taifa Jumapili imebaini kwamba kinyume na ripoti nyingi kuwa ni kampuni ya Cambridge Analytica pekee iliyotumiwa kubadilisha hisia za wapigakura nchini, kampuni nyingine saba zilishirikiana kisiri na kampuni hiyo kuhakikisha Jubilee ingeendelea kuba- ki mamlakani.
Kwa kutumia mfumo maalum wa teknolojia ambao ulibuniwa katika Chuo Kikuu cha Cambridge, Uin- gereza kufanyia utafiti, kampuni hizo zilikuwa zikiun- ganisha maelezo ya mtu binafsi ambayo ameandika kwenye akaunti yake ya Facebook.
Vile vile, ziliunganisha maelezo hayo na marafiki ambao mtu yuko nao kwenye mtandao. Kupitia ujuzi wa kiteknolojia, kampuni hizo zilitathmini kwa kina maelezo kutoka kwa watu wali- omuunga mkono Bw Odinga na kubuni mbinu mbal- imbali za kubadili matokeo ya mwisho ya kura.
“Hilo lilizisaidia kampuni kufahamu sifa za ndani za wapigakura, kama miegemeo yao kisiasa, kijamii, kiwango cha imani yao kwa wanasiasa maarufu na malengo yao kwenye upigaji kura,” akasema Bw Tim- othy Oriedo, ambaye ni mkuu wa shirika la Predictive Analytics Lab, linalohusika kwenye utathmini wa data na maelezo mitandaoni.
Kampuni hizo zilitumia maelezo ziliyopata kuwa- tumia watu matangazo ya kisiasa yaliyowahusu vion- gozi waliowaunga mkono. Kupitia mbinu hiyo, wale ambao walimuunga mkono Bw Odinga wangepokea jumbe kwenye Facebook zikiwa kwa mfumo wa video fupi zilizomsawiri kama kiongozi ambaye hakufaa kuwa rais.
Vyombo vya habari vyenye ushawishi na vile am- bavyo havina ushawishi pia vilitumiwa kubadilisha mitazamo ya wapigakura dhidi ya Bw Odinga. Hilo ndilo linatajwa kuchangia ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta.
Kupitia mkakati maalum, dhana hiyo ilitumwa kwa vyombo vya habari na wanablogu kuangazia pakub- wa kampeni ya Jubilee ikilinganishwa na ya Bw Odinga.
Vivyo hivyo, wadadisi wanasema kuna uwezekano mkubwa mbinu kama hizo kurudiwa tena kwenye uchaguzi mkuu wa 2022.
“Hatuwezi kuondoa uwezekano wa mbinu hizo kutumika tena 2022. Mashirika mengi yanafuatilia kwa karibu mielekeo ya kisiasa nchini ambapo huenda ya- kaahidi “kuwasaidia” baadhi ya wanasiasa,” akasema mdadisi wa siasa ambaye hakutaka kutajwa.
Majuzi, kundi moja la wanaharakati nchini Amerika lilieleza tashwishi ikiwa uchaguzi mkuu wa 2022 utakuwa wenye uwazi.
Kundi hilo lilifichua jinsi Facebook imekuwa ikieneza habari za uongo kwa watumizi wake zaidi ya 3.8 bilioni kote duniani.
Hapo awali, Facebook iliiruhusu kampuni hiyo kuchukua na kutumia maelezo ya watu binafsi nchini kuathiri matokeo ya chaguzi za 2013 na 2017.
Mnamo Machi 2018, makala moja ya kipekuzi ilimwonyesha Mkurugenzi Mkuu wa Cambridge Analytica, Mark Turnbull akijipiga kifua kuhusu jinsi walivyotumia mbinu chafu za kisiasa kuathiri matokeo ya chaguzi za 2013 na 2017. Alisema walipewa jukumu hilo na chama cha Jubilee.