• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 6:50 AM
‘Mugabe angali na funguo za ofisi ya Ikulu’

‘Mugabe angali na funguo za ofisi ya Ikulu’

Na AFP

ALIYEKUWA rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, angali anashikilia funguo za mojawapo ya afisi muhimu ya serikali katika Ikulu.
Hayo yanafichuka miezi minne baada ya kiongozi huyo kulazimika kung’atuka uongozini.

Kulingana na Msemaji wa Rais Emmerson Mnangagwa, George Charamba, juhudi za kumshinikiza Mugabe kurudisha funguo hizo zinaonekana kugonga mwamba.

“Kuna ukweli ambao hatuwambii wananchi kwamba Bw Mugabe angali anaendelea kushikilia funguo za afisi muhimu katika Ikulu,” akasema Bw Charamba, kwenye mahojiano na gazeti la ‘Standard.’

Madai hayo yanajiri baada ya habari kuibuka kwamba baadhi ya vipakatalishi ambavyo viliwekwa na familia ya Bw Mugabe katika mojawapo ya afisi katika Ikulu vilipotea katika hali tatanishi.

Familia ya Bw Mugabe imekuwa ikishikilia kwamba iliikabidhi serikali mpya “kila kitu.”

Lakini Bw Charamba aliitetea vikali serikali ya Rais Mnangagwa, akiyataja madai ya familia ya Bw Mugabe kuwa “uongo mtupu.”

“Rais Mnangagwa hajaingia katika afisi husika. Je, ni vipi anaweza kuingia katika afisi ambayo hana funguo zake?” akashangaa.
Bw Mugabe, ambaye ana umri wa miaka 94, alilazimika kung’atuka uongozini baada ya jeshi kuitwaa serikali.

 

You can share this post!

Jeshi laokoa wanawake 54 na watoto 95 kutoka Boko Haram

SHANGAZI: Iweje wananishuku ilhali ‘mali’ nimetia...

adminleo