Makala

KIKOLEZO: Je, TPF lilikuwa shindano la mkosi?

November 20th, 2020 1 min read

Na THOMAS MATIKO

JUMA lote hili imetrendi stori ya masaibu anayopitia staa wa zamani wa shindano la uimbaji la Tusker Project Fame lililokuwa maarufu sana zaidi ya miaka sita, saba iliyopita.

 

Esther Nabaasa. Picha/ Hisani

Ukweli mchungu ni kwamba TPF haikuchangia kuwatoa mastaa wa uimbaji kama ilivyodhamiriwa.

Ni wachache sana walioishia kutoboa kwenye muziki baada ya kushiriki TPF.

Wengi wa washiriki waliishia kuwa vichekesho na hata wengine walishasahaulika kabisa. Je, TPF lilikuwa shindano la mikosi?

Ruth Matete. Picha/ Hisani