MakalaShangazi Akujibu

Mke wangu hunitishia kwa kisu tunapogombana

Na SHANGAZI April 3rd, 2025 Kusoma ni dakika: 1

SWALI: Kwako shangazi, hujambo? Wiki iliyopita tuligombana na mke wangu, na akachukua kisu akinitishia kuniua.

Hii si mara ya kwanza kufanya hivyo; kila anapokasirika, hunilenga kwa chochote kilicho karibu.

Nimechoka kuishi katika hofu na ninahisi njia pekee ni kuachana naye. Naomba ushauri wako.

JIBU: Sijambo, nashukuru. Tabia ya kutumia vurugu au vitisho ni hatari na inakiuka misingi ya heshima katika ndoa. Usalama wako ni muhimu.

Tafuta msaada wa haraka kutoka kwa mshauri wa familia au shirika linaloshughulikia masuala ya unyanyasaji. Ikishindikana, chukua hatua za kisheria au umpe talaka ili kulinda maisha na ustawi wako wa kiakili.