• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Gor Mahia yarejea nyumbani na kumulika ligi kuu

Gor Mahia yarejea nyumbani na kumulika ligi kuu

Na GEOFFREY ANENE

MIAMBA wa Gor Mahia walirejea nchini mapema Jumatatu kutoka Libya, huku mashabiki wao wakichochea mabingwa hao wa Ligi Kuu kuonyesha kivumbi Kakamega Homeboyz watakaporejea uwanjani Novemba 21.

Gor ya kocha Steven Polack ilialikwa na mabingwa wa zamani wa Libya, Al Hilal Benghazi kwa mechi ya kirafiki, ambayo ripoti zinasema ilikuwa ya kwanza dhidi ya timu ya kigeni kufanyika nchini humo tangu Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) lizime nchi hiyo kuandaa mechi za kimataifa mwaka 2011 kutokana na hali tete ya usalama.

Vijana wa Polack walikaba Al Hilal 1-1 uwanjani Benina mnamo Novemba 16.

Samuel Onyango alisawazishia Gor dakika ya 34 baada ya Ali Alsharif kupatia Al Hilal bao la mapema katika dakika ya tano.

Gor inaongoza ligi hii ya klabu 18 kwa alama 18 kutokana na mechi saba. Iko alama moja mbele ya Homeboyz, ambayo imesakata mechi mbili zaidi.

Timu hizi zitakutana uwanjani Moi mjini Kisumu baada ya Gor kutangaza juma lililopita kuwa itarejesha mechi zake katika uwanja huo kutokana na mapato ya chini ikialika wapinzani katika viwanja vingine.

You can share this post!

Harambee Starlets mawindoni kuzoa ushindi dhidi ya Djibouti

Kabras, KCB na Homeboyz wanyimana pumzi Kenya Cup

adminleo