• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 5:41 PM
JUNGU KUU: Mafanikio maishani hayapatikani kwa njia ya miujiza au ndoto!

JUNGU KUU: Mafanikio maishani hayapatikani kwa njia ya miujiza au ndoto!

Na WALLAH BIN WALLAH

LEO ni wiki moja kamili tangu gazeti letu la Taifa Leo lilipozinduliwa likapata sura mpya tunayoiona hivi sasa!

Katika makala haya nimedhamiria kueleza kwa ufupi tu kuhusu siri ya mafanikio maishani kwa sababu watu wengine wanadhani ati mafanikio ya kweli hupatikana kwa miujiza au kama ndoto tu!

Mafanikio ya kweli hutokana na bidii, uvumilivu na kujituma kwa hali na mali maishani! Kufanikiwa ni sawa na mazao ya mbegu alizopanda mtu shambani kisha akavuna!

Ndipo leo nakudokezea kwamba, ukitaka kuvuna haraka haraka, panda UYOGA uvune siku hiyo hiyo! Na ukishauvuna, uyoga huo utaoza siku hiyo hiyo!

Ukitaka mavuno ya miezi miwili, panda maharage! Ukitaka mavuno ya miezi minne hadi sita, panda mahindi! Na ukitaka uvune kila baada ya mwaka mmoja, panda miti ya matunda kama vile miembe, michungwa, mipera, miparachichi na mingineyo!

Lakini ukitaka mavuno ya kudumu katika maisha yako yote enda ukapande mbegu ya ELIMU! Utavuna kila siku! Na lazima ujue kwamba elimu hupatikana tu kwa uvumilivu, bidii na kujituma kusoma vitabu, magazeti, majarida na kuwatii walimu wakufundishao shuleni!

Ndugu wapenzi, mtu anayeogopa kukaa shuleni kusoma afundishwe ili apande mbegu ya ELIMU kichwani, atajifunza vipi?

Mja ambaye anachoma shule ambayo ndiyo chemchemi ya elimu, atasomea wapi? Lini? Hajui kwamba kila mtu atavuna alichopanda?

You can share this post!

Mshukiwa katika kesi ya Obado ajifungua huku bintize...

Kesi dhidi ya mbunge wa Wajir mashariki yatamatishwa

T L