• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 9:35 PM
Manchester City guu moja ndani ya nusu-fainali UEFA

Manchester City guu moja ndani ya nusu-fainali UEFA

NA MASHIRIKA

MANCHESTER, Uingereza

MANCHESTER City wameweka guu moja ndani ya nusu-fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) baada ya kuicharaza Bayern Munich kwa 3-0, Jumanne usiku.

Kwa upande mwingine, Bayern Munich wana kibarua kigumu cha kufuzu kwa hatua hiyo licha ya kocha wao kusisitiza kwamba kikosi chake kina uwezo wa kulipiza kisasi na kugeuza matokeo hayo katika mechi ya marudiano mnamo Aprili 19.

Alipoulizwa iwapo timu yake ina uwezo wa kuifunga Manchester City katika mechi ya marudiano itakayochezewa Allianz Arena, Thomas Tuchel wa Bayern alisema vijana wake lazima wapambane hadi dakika ya mwisho wakilenga ushindi.

Kwenye mechi hiyo iliyochezewa Etihad Stadium, mabao ya washindi yalitiwa wavuni na Rodri dakika ya 27, Bernardo Silva na Erling Haaland ambaye sasa amevunja rekodi ya ufungaji mabao ndani ya msimu mmoja.

Tangu ligi kuu ya Uingereza igeuze jina na msimu wa 1992-93 na kuitwa Ligi Kuu ya Premia (EPL) hakuna mchezaji wa ligi hiyo maarufu aliyewahi kufunga mabao 45 kwa msimu mmoja katika mashindano tofauti hadi sasa.

Ruud van Nisterlrooy alifunga 44 akiwa na Manchester United msimu wa 2002-03, sawa na Mohamed Salah wa Liverpool aliyefanya hivyo msimu wa 2017-18.

Van Nistetrooy na Salah walifunga mabao yao kutokana na mechi 52. Haaland ameivunja rekodi hiyo kutokana na mechi 13 pekee.

Nistelrooy alifunga mabao yake katika msimu wa pili baada ya kujiunga na United, wakati Salah akifanya hivyo kwa mwaka wa kwanza pale Anfield akitokea Chelsea.

Huku timu zote zikifanya vizuri kwenye ligi zao za nyumbani, Pep Guardiola atakuwa akilenga kumzima Tuchel ambaye aliongoza Chelsea kulaza kikosi chake katika fainali ya michuano hiyo mnamo 2021.

Hata hivyo, vigogo hao wa Ligi Kuu ya Premia (EPL) watalazimika kuonyesha kiwango cha juu mjini Munich kama wangetaka kuendeleza ubabe wao msimu huu.

Langoni mwa Bayern kulikuwa na kipa mgeni Yann Sommer aliyechukuwa mikoba kutoka kwa mkongwe Manuel Neuer alistaafu kucheza kutokana na ajali iliyotokana na kuteleza kwa barafu.

Licha ya kuwa mechi yake ya kwanza kubwa, Sommer aliokoa hatari nyingi kutoka kwa washambuliaji wa Man-City, sawa na mwenzake Ederson wa Man-City aliyezuia mipira ya vichwa kutoka kwa Matthijs de Light na Kingsley Coman.

Kwingineko, Romelu Lukaku alifunga penalti dakika ya 82 na kusaidia Inter Milan kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Benfica na kujiongezea matumaini ya kushinda mechi ya marudiano.

Nicolo Barella alifunga bao la kwanza la Inter Milan katika mechi hiyo iliyochezewa Lisbon, mbele ya mashabiki wengi wa Benfica ambao wana kibarua kugumu cha kubadilisha matokeo hayo.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Vizingiti vya mazungumzo viondolewe

Familia yahofia ‘pepo wa mauti’ huwafyeka...

T L