Kimataifa

Michael Jackson alipenda kujichua akitumia Vaseline – Kijakazi

February 13th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

MASHIRIKA Na PETER MBURU

ALIYEKUWA kijakazi wa msanii tajika marehemu Michael Jackson ametoboa kuwa bingwa huyo wa muziki alikuwa ametundika picha za watoto walio uchi nyumbani kwake shamba la Neverland na alipenda kusoma vitabu kuhusu kujichua.

Bi Adrian McManus wa miaka 56 alidai kuwa msanii huyo wakati mmoja alimwagiza kuzihifadhi picha hizo na kuzitundika kwenye ukuta wa chumba cha kulala, ili ‘kuurembesha.’

Adrian alisema kuwa mwanamuziki huyo aliwadhulumu makumi ya watoto na kuchukua filamu yake akiwatendea vitendo hivyo vya aibu, kisha kuhifadhi kanda za video katika maktaba ya siri.

Bi McManus alifanya kazi nyumbani kwa marehemu Jackson kwa miaka minne kutoka 1990 na alikiri kuwa aliwaona watoto wachanga wakitembea nyumbani huko, bila mavazi. Alisema alikuwa akiokota nguo za ndani za msanii huyo na watoto kando ya kitanda chake.

Alidai kuwa kila mara, Jackson angekuwa na picha za watoto na mafuta ya Vaseline vyote vikitapakaa nyumbani, alipokuwa akijichua.

Akizungumza kuhusu kanda za video alizokuwa akihifadhi kisiri, Bi McManus alisema “nadhani zilikuwa za Michael na wavulana wakifanya vitendo vya aibu ambavyo lazima vingefichwa, ama vingempeleka jela. Nadhani zilikuwa kanda za ngono.”

Alisema kuwa walinzi wa Jackson walimtishjia kuwa wangelipa mtu kumuua ikiwa angetoboa chochote kuhusu matukio hayo, ndipo akaamua kunyamaza kwa muda mrefu.

Wanaume kadha wamejitokeza kudai kuwa msanii huyo aliwahi kuwalawiti walipokuwa wavulana wachanga, Bi McManus akisema hakushangaa aliposikia hivyo.

Katika uhai wake, Jackson aliishi kupinga madai hayo kuwa aliwadhulumu kingono watoto. Polisi walivamia nyumbani kwake katika shamba la Neverland mnamo 2003 walipokuwa wakichunguza kisa kuwa alimlawiti mvulana wa miaka 13, katika kesi ambayo iliangaziwa sana Marekani.

Hata hivyo, walipofika kortini, mvulana huyo alibadili ushahidi na kusema kuwa Jackson hakuwahi kumlawiti. Msanii huyo aliachiliwa na korti mnamo 2005.