KASHESHE: Mafisilet jomba ni singo…
Na THOMAS MATIKO
MWANAMUZIKI mpenda skendo Willy Paul, kadai kuwa wanawake wamemshinda kabisa hivyo suala la kuwa kwenye mapenzi limebaki kuwa stori kwake.
Ijapokuwa ni msanii wa injili, Willy Pozee anafahamika kwa tabia yake ya kuwabadili mademu kila kukicha japo anafanya kwa usiri sana.
Hivi majuzi, alifunguka na kusema haamini kabisa kwenye suala la mapenzi kwa sababu wanawake ni wagumu kuwaelewa.
“Kwa sasa sipo kwenye uhusiano wa kimapenzi ingawaje nafahamu kuwatungia nyimbo za mapenzi. Wanawake ni watu wagumu sana ku-deal nao. Haya sio maamuzi yangu ila vitu ambavyo maisha yamenifunza kuwahusu. Ndio maana siamini katika mapenzi,” Pozee kafunguka.
Kauli yake inatoka kipindi demu anayedaiwa kuwa ‘baby mama’ wake Mali Queen kuwataka mafisilet waachane na dume lake.