Habari za Kitaifa

HABARI ZA HIVI PUNDE: Jengo la ghorofa 13 laporomoka Eastleigh

Na BENSON MATHEKA October 23rd, 2026 Kusoma ni dakika: 1

Waokoaji kutoka Idara za kukabiliana na  Dharura na Majanga Kaunti ya Nairobi wameanzisha shughuli za kutafuta na kuokoa watu baada ya jengo la ghorofa 12 lililokuwa likijengwa kuporomoka Eastleigh, Nairobi.

Jengo hilo lililoko kwenye makutano ya First Avenue na 9th Street lilikuwa bado linaendelea kujengwa, huku ghorofa ya chini ikiwa tayari inatumiwa.

Taarifa kutoka kwa kaunti zinaonyesha kuwa huenda baadhi ya watu wamenaswa chini ya vifusi kufuatia tukio hilo.

Timu za uokoaji zimefika eneo la tukio na zinaendelea kutathmini hali huku zikifanya msako wa kuwatafuta watu wanaoweza kuwa wamefunikwa na kifusi.

Mashine nzito zimepelekwa kusaidia kuondoa vifusi na kufungua njia ili waokoaji kufikia maeneo ambayo huenda waathiriwa wamekwama.

Hata hivyo, taarifa kuhusu idadi ya watu waliojeruhiwa, waliokufa au waliookolewa hazikuwa zimepatikana kufikia wakati wa kutolewa kwa taarifa hiyo.

Kaunti imesema itatoa taarifa zaidi kadiri operesheni ya uokoaji inavyoendelea na habari mpya kupatikana.