• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Faida ya Kenya Power yashuka

Faida ya Kenya Power yashuka

Na BERNARDINE MUTANU

FAIDA ya kampuni ya Umeme nchini (Kenya Power) imeshuka kwa asilimia 30.3.

Hii ni baada ya kupata mapato baada ya ushuru ya Sh2.97 bilioni ikilinganishwa Sh4.2 bilioni katika kipindi kama hicho 2016.

Wikendi, kampuni hiyo ilisema hali hiyo ilitokana na kudhoofika kwa uchumi na ongezeko la gharama ya operesheni zake.

Katika notisi kwa vyombo vya habari, shirika hilo lilisema mauzo yaliongezeka kwa asilimia 2.3 kutoka gigawati 3,805 mwaka wa 2016 hadi gigawati 3,893 kufikia Desemba 31, 2017.

Mapato kutokana mauzo yaliongezeka hadi Sh46.93 bilioni kutoka Sh45.79 bilioni 2016.

Gharama ya operesheni iliongezeka hadi asilimia 17.37 baada ya kutumia Sh8.78 bilioni zaidi ya 2016 ambapo ilitumia Sh50.54 bilioni.

Gharama ya usambazaji wa umeme iliongezeka kwa asilimia 5 kutoka Sh15.1 bilioni hadi Sh15.82 bilioni, ilisema Kenya Power.

Kushuka kwa mapato kulitangazwa wakati ambapo wanalalamikia ongezeko la bei ya matumizi ya umeme.

You can share this post!

Tobiko aunda jopokazi la kulinda misitu

Hali ngumu ya uchumi yashusha uzalishaji wa saruji

adminleo