• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:40 AM
Ndani miaka 25 kwa kufuja pesa za CDF

Ndani miaka 25 kwa kufuja pesa za CDF

Na GERALD BWISA

MAHAKAMA moja ya Kitale Jumanne iliwahukumu wanachama wawili wa iliyokuwa kamati ya usimamizi wa fedha za Hazina ya CDF ya Eneobunge la Saboti kifungo cha miaka minane gerezani kwa madai ya kufuja fedha au faini ya Sh2.1 milioni kila mmoja.

Mwanachama mwingine alihukumiwa kifungo cha miaka tisa, au kulipa faini ya Sh2.4 milioni.

Watatu hao walihukumiwa kwa kufuja fedha zilizopangiwa kutumika katika miradi ya maendeleo.

Hakimu Mkuu wa Kitale, Valentine Wandera aliwapata washtakiwa Ignatius Katasi Maina, Charles Maina na Thaddaeus Wekesa na makosa ya ufujaji wa fedha hizo miaka 11 iliyopita.

Walishtakiwa pamoja na Isaac Masengeli, ambaye hakuwa mahakamani. Mshtakiwa huyo angali anatafutwa na Tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi (EACC).

Watatu hao walishtakiwa kwa kufuja Sh700,000 kutoka hazina hiyo, ambazo zililenga kugharamia uchimbaji wa kisima cha maji katika Shule ya Upili ya Nabunga mnamo 2007.

 

You can share this post!

Mwanaume ajuta kumuua mwanawe na kusulubisha mwili kama Yesu

NLC yashindwa kuelezea ziliko Sh2 bilioni

adminleo