• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Mamia ya wakazi waachwa gizani na Kenya Power msakoni Tassia

Mamia ya wakazi waachwa gizani na Kenya Power msakoni Tassia

Na BERNARDINE MUTANU

Kampuni ya Kenya Power imewaacha bila stima wakazi wa orofa 20 katika mtaa wa Tassia, Nairobi wakati wa operesheni kali.

Operesheni hiyo ilianzishwa kumaliza matumizi haramu ya umeme na makachero wa kampuni hiyo wakishirikiana na maafisa wa kutoza ushuru na maafisa wa polisi.

Kampuni hiyo imekuwa ikifanya kampeni hiyo kwa muda sasa kumaliza uharibifu wa vifaa vya umeme, wizi wa stima na wizi wa nyaya za stima na transfoma.

“Wizi wa stima uhatarisha maisha ya wanaofanya hivyo na pia wale wanaowekewa. Tunataka kuhakikisha kuwa tumemaliza wizi wa stima na vifaa,” alisema meneja wa eneo la Nairobi Kusini Bw Aggert Machasio.

Alisema watakaopatikana watakamatwa na kufunguliwa mashtaka mahakamani.

Msimamizi huyo aliongeza kuwa wizi huo ulikuwa umeipunguzia kampuni hiyo mapato, na husababisha umeme kupotea.

You can share this post!

Msako dhidi ya Al-Shabaab msituni Boni waanzishwa

Kiwanda kipya cha gesi kujengwa Murang’a

adminleo