• Nairobi
  • Last Updated March 19th, 2024 10:55 AM
Kamata kamata ya polisi kwa wasiovalia maski Krismasi ikianza

Kamata kamata ya polisi kwa wasiovalia maski Krismasi ikianza

Na SAMMY WAWERU

Maafisa wa polisi jijini Nairobi na viunga vyake wanaendeleza msako mkali kwa wanaopuuza kuvalia maski wakiwa katika maeneo ya umma.

Msako huo umejiri baada ya Inspekta Mkuu wa Polisi, IG, Hillary Mutyambai mnamo Jumanne kuagiza maafisa wa polisi kote nchini kuchukulia hatua wananchi wanaopuuza sheria na mikakati iliyowekwa na Wizara ya Afya kusaidia kudhibiti msambao wa Covid-19, hasa msimu huu wa Krismasi.

“Saa za kuanza kwa kafyu ya kitaifa ni saa nne usiku, kila mmoja awe kwenye nyumba,” IG Mutyambai akasema, wakati akihutubia wanahabari katika afisi yake Jogoo House Nairobi.

Idara ya askari wa magereza imeahidi kuungana na maafisa wa polisi kutekeleza sheria na mikakati kuzuia kuenea kwa virusi vya corona msimu wa Krismasi, Kamishna Mkuu wa idara hiyo, Wycliffe Ogalo akitangaza kushirikisha maafisa kadha.

Mitaa ya Roysambu, Zimmerman na Githurai tayari maafisa wa polisi wameanza kupiga doria, bila kuvalia sare na kukamata wanaopuuza kuvalia barakoa.

Aidha, kufikia jana jioni kituo cha polisi cha Zimmerman kilikuwa kimewatia nguvuni watu kadhaa.

Baadhi ya waliokamatwa walikuwa na maski, ila kwenye mifuko, wengine wakiikamata mkononi. Faini ya kutovalia barakoa katika maeneo ya umma ni Sh20, 000.

You can share this post!

Ruto akutana na Feisal baada ya kushinda kiti cha Msambweni

Wakenya wengi wana matumaini ya 2021 kuwa bora –...