Dondoo
Kidosho anyima wifi yake chai kwa kudai humsengenya kwenye saluni
MWANADADA mmoja katika kijiji cha Murumba kilichoko Budalang’i, Kaunti ya Busia, alikashifiwa vikali kwa kumnyima wifi chai akidai alimsengenya kwenye saluni.
Mwanadada alitembelewa na dada ya mumewe kumjulia hali. Hata hivyo, safari yake ilionekana kumletea machungu baada ya mwenyeji wake kumnyima chai.
“Nilidhani wewe ni mama wa heshima ambaye ungenitia moyo nilinde ndoa, kumbe wewe ni wifi usiye na adabu. Unanisengenya kisha unakuja hapa kujifanya mzuri. Sikutaki!” mwanadada alifoka.