Walevi wawakia pasta kwa kuingilia starehe zao
WALEVI kutoka eneo hili la Mayamachaki, Kaunti ya Nyeri, walimuonya pasta mmoja dhidi ya kuingilia maisha yao.
Walevi hao walielekea hadi kwa boma la pasta na kumpa onyo kali bila woga.
“Wewe ni pasta na tunakuheshimu. Kile unamuambia mamapima koma kabisa. Hakuna siku tumetumia pesa zako kwa ulevi,” makalameni walimfokea pasta.
Duru zinasema hapo awali pasta alikuwa amewashawishi makalameni kuachana na ulevi ili wajiunge na kanisa lake.
Inadaiwa aliposhindwa kuwashawishi, pasta alimueleza mamapima akome kuwauzia makalameni hao pombe.
“Sisi tunakula mali yetu polepole kwa mamapima. Wewe pia ukitaka unaweza kujiunga nasi ule sadaka polepole,” pasta alizomewa.