Lita 4,500 za Dizeli ya soko la nje zanaswa Kisumu
Na BERNARDINE MUTANU
TUME ya Kudhibiti Mafuta nchini (ERC) Ijumaa imetoa taarifa kuhusu operesheni kumaliza biashara haramu ya mafuta eneo la Otonglo, Kaunti ya Kisumu.
Operesheni hiyo ilifanywa Jumatano na maafisa wa uchunguzi wa kihalifu (DCI) na police wa GSU ambao walipata lita 4,500 za dizeli ya kuuza nje.
Wakati wa operesheni hiyo, washukiwa watano walikamatwa na gari lenye nambari ya usajili KAN 022 C. Watano hao walifikishwa mahakamani Jumatano na kushtakiwa kwa kuendesha biashara bila leseni kinyume cha sheria.
Kituo hicho pia kiliharibiwa kwa mujibu wa sheria, ilisema ERC.