FBI wavamia ofisi ya wakili wa Trump kuhusu ulaghai na filamu za ngono
Na CHRIS ADUNGO
WASHINGTON, AMERIKA
KIKOSI maalum cha polisi, FBI kimevamia ofisi ya wakili wa kibinafsi wa Rais Donald Trump, Michael D. Cohen (pichani) katika Kituo cha Rockefeller usiku wa kuamkia Jumanne na kutwaa rekodi za biashara, baruapepe na stakabadhi kuhusu mada mbalimbali ikiwemo malipo ya filamu za ngono.
Lakini Rais Trump katika mrejesho wake wenye ghadhabu, alikejeli hatua hiyo baada ya kuibuka kuwa ofisi hiyo ilivunjwa ili kumchunguza wakili huyo kuhusu madai ya ulaghai wa benki.
Bw Trump aliisuta Idara yake ya Haki akisema hatu ahiyo inaongozwa na lengo fiche na kusisitia kuwa maafisa wa F.B.I ‘walivunja’ ofisi ya Bw Cohen.
Rais huyo aliyeongea katika ofisi yake ya White House, kabla ya ya kukutana na makamanda wa ngazi ya juu kuhusu uwezekano wa Amerika kuvamia Syria, alitaja uvamizi wa F.B.I kuwa “kitendo cha aibu” na “shambulizi la kikweli dhidi ya nchi yetu.”
Haijabainika iwapo maafisa hao walijitoma ndani ya ofisi ya Bw Cohen, lakini maajaenti hao walikuwa na kibali cha kuchakura ofisi hiyo, na hivyo wangewaarifu wafanyakazi wa hoteli hiyo kuwakubalia kuingia.
Stakabadhi zinaonyesha kibali hicho kilitolewa miaka mingi iliyopita.
Malipo yaliyotolewa kwa muigizaji wa filamu za ngono, Stephanie Clifford, anayejulikana kama Stormy Daniels, ni moja kati ya mda nyingi ambazo zinachunguzwa na FBI.
Kibali hicho ni mojawapo ya mbinu zinazotumiwa na viongozi wa mashtaka kuingilia biashara za siri za Rais Trump, na kinamkosesha usingizi.