• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Mwalimu ajiua kwa kukataliwa na ex, aacha mke mjamzito

Mwalimu ajiua kwa kukataliwa na ex, aacha mke mjamzito

NA GEORGE MUNENE

MWALIMU wa shule ya sekondari kutoka kijiji cha Nthangathiri, Kaunti ya Embu, alijitia kitanzi ndani ya nyumba yake baada ya mpenzi wake wa pembeni kumtema.

Marehemu aliyetambulishwa na polisi kama Dennis Mwaniki Njeru, 32, almaarufu kama Mukono, alipatikana amelala kwenye kitanda chake na barua aliyoandika kando yake.

Kulingana na polisi, marehemu alikuwa anavuja povu kupitia pua lake huku kemikali inayoshukiwa kuwa dawa ya kuua wadudu ikipatikana humo vilevile.

“Ni mwalimu kutoka Mbeere Kaskazini lakini anafunza katika shule ya Sekondari iliyopo Kaunti ya Kirinyaga, alipatikana akiwa amekufa nyumbani kwake. Uchunguzi wa awali umeonyesha alijtoa uhai,” alisema.

Kwenye kijikaratasi hicho, mwendazake alisema alichukua uamuzi huo baada ya mpenziwe kumkataa.

“Naweza nikaonekana mjinga lakini nimefungua moyo wangu kuhusu kinachoniumiza kwa watu 17 lakini hakuna aliyezungumza nami, acha tukutane mbinguni. Nimemsihi mpenzi wangu lakini yote yameambulia patupu. Nawapenda nyote,” alisema kupitia barua hiyo.

Bw Njeru vilevile ameacha maagizo kuhusu jinsi anavyotaka kuzikwa.

Ameagiza afisa mkuu katika Bunge la Kaunti pamoja na diwani wa eneo hilo kuongoza mipango ya mazishi yake.

Aidha, alisema azikwe Sikukuu ya Wapendanao almaarufu kama Valentine ambapo mpenzi wake anapaswa kusoma wosia.

  • Tags

You can share this post!

Lupita Nyong’o azungumzia ugumu wa kuandaa filamu ya...

Waziri ajiuzulu kufuatia upungufu wa pombe

T L