• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 10:30 AM
Kizaazaa babu aliyeenda kununua mahaba kugundua mtumbuizaji ni mjukuu wake damu moja

Kizaazaa babu aliyeenda kununua mahaba kugundua mtumbuizaji ni mjukuu wake damu moja

NA MWANGI MUIRURI

Kulizuka kizazaa Ijumaa ya Desemba 1 katika lojing’i moja ya Kaunti ya Kirinyaga baada ya babu aliyekuwa ameenda kununua mahaba kupata mjukuu wake ndiye kahaba mpokezi.

Kwa mujibu wa mdokezi wetu katika mtaa wa Makutano ulioko katika mpaka wa Kaunti za Embu, Kirinyaga, Murang’a na Machakos, babu alipiga nduru huku akilaani baada ya kugundua hali ilikuwa si hali tena.

“Ilivyo ni kwamba, makahaba huwa wamekodisha vyumba ndani ya lojing’i na kisha wakiwa wamevalia nusu uchi, hungojea wateja waingie biashara iive,” akasema mdokezi wetu.

Ni katika hali hiyo ambapo babu ambaye ni mwalimu mstaafu wa miaka 64 alifika ndani ya lojing’i moja akitaka raha kwa kipimo cha Sh200.

“Mimi nilimwona Mzee huyo ameingia kwa chumba kimoja na mlango ukafungwa. Muda kidogo nikamsikia alipiga nduru huku akiita majina ya miungu wa kwao,” bawabu wa lojing’i hizo akasimulia.

Aliongeza kuwa kufika katika chumba hicho na kubisha, Mzee ndiye alifungua mlango huku akiwa uchi kuanzia kiuno kuteremka.

“Msichana naye alikuwa amejifunika kwa blanketi huku akilia. Tuliuliza kulikoni na ndipo babu alikiri kwamba msichana huyo alikuwa ni mjukuu wake wa miaka 17 pekee na aliyekuwa amekataa masomo miaka miwili iliyopita,” akasema bawabu.

Aliongeza kuwa babu alifika ndani ya chumba hicho lakini akashtuka alipoona msichana aliyekuwa ameficha uso ndani ya blanketi.

“Kumfungua ndio ajue ni kwa nini msichana alikuwa ameficha uso ndipo alikumbana na ushahidi kwamba babu tayari alikuwa ameanika uchi wake wake mbele ya uso wa mjukuu wake,” akasema mdokezi.

Mzee alikuwa akilia akihoji atatekeleza tambiko gani bila ya kuanika uasherati wake na pia kutakasa aibu ya kuonwa uchi kimakusudi na mtoto wa kike wa bintiye.

“Kila aliyesikia stori hiyo alikiri kwamba hali ilikuwa tatanishi na iliyohitaji Mungu pekee kuitatua. Sisi tuliambia babu atoke mahali hapo na aende akatafute suluhu la masaibu yake katika usiri wa boma lake,” akasema mdokezi.

Msichana naye alipata pigo la kuona kiungo kilichoshirikiana na kile cha nyanyake kumleta mamake ulimwenguni na kisha naye akamzaa.

“Msichana alitimuliwa kutoka kwa lojing’i hiyo kwa msingi kuwa alikuwa mtoto wa miaka 17…tulihofia kuandamwa na polisi wakifikiwa na kisanga hicho…Ni kisa ambacho kimezua mjadala mkali hapa Makutano,” akasema mdokezi.

  • Tags

You can share this post!

Arati kwenye kinywa cha mamba Naibu wake akiungana na...

Kimeumana nyumbani kwa Neymar, mpenziwe aliyejifungua juzi...

T L