Makala

MAWAIDHA YA KIISLAMU: Kudumu na ibada baada ya Saumu ni ishara ya kukubaliwa funga yako

June 7th, 2019 Kusoma ni dakika: 3

Na HAWA ALI

SIFA zote njema anastahiki Mola Azzawajalla, swala na salamu zimwendee kipenzi cha Umma, Mtume Muhammad (SAW).

Allah anasema; “Na Muhammad si yeyote isipokuwa ni Mtume tu. Wamekwishapita kabla yake Mitume. Je, akifa au akiuawa mtageuka nyuma ya visigino vyenu (mrudi ukafirini)? Na atakayegeuka nyuma ya visigino vyake, basi hatomdhuru Allah kitu chochote. Na Allah ata walipa wenye kushukuru. Na unaelewa nini unaposoma Hadithi ya Mtume iliyorekodiwa na Imamu Bukhari na Muslim kutoka kwa Anas ambapo aliele- za kuwa Mtume wa Allah (rehe- ma na amani ya Allah imshukie) alisema: “Mambo matatu atakayekuwa nayo, atapata uta- mu wa Imani; Allah na Mtume Wake wawe vipenzi zaidi kwake kuliko wengineo, ampende mtu na wala asimpende isipokuwa kwa ajili ya Allah, na achukie ku- rudi katika ukafiri baada ya Allah kumuokoa kutoka huko kama anavyochukia kuingizwa motoni”.

Naam; kwa watu wengi ibada walizokuwa wakizifanya katika Mwezi wa Ramadhani zitaishia siku ya Idd sawa kabisa na mbio za sakafuni.

Mpenzi msomaji. mafunzo ya ibada ya Swaumu yanakusudiwa kubakia na kutekelezwa na kila mmoja wetu baada ya kumalizika kwa chuo hiki adhimu kwa muda wote utakaofuatia baada ya Ramadhani. Hebu tujikumbushe kidogo falsafa ya Ramadhani.

Kwanza kabisa, suala zima la kujizuwia na kula, kunywa na matamanio ya kiwiliwili kutoka alfajiri hadi magharibi tunapata mafundisho maalumu.

Katika mafunzo hayo ni pamoja na: Utulivu na upole, kuwa na tafakuri, kuishi ndani ya Qur’an, kuwafikiria waja wenzetu na hali ya Ummah wa Kiislamu kwa ujumla, kujiweka mbali na mapambo na matamanio ya vitu vya kidunia.

Mafunzo haya na neema nyingi yanatuwezesha, kwa uwezo wa Allah, kutupa faida ya hali ya juuyauvumilivunaustahamilivu katika nafsi zetu. Allah anasema katika Qur’an: “Enyi mlioamini! Takeni msaada kwa subira na swala. Hakika Allah Yu pamoja na wanaosubiri,” (Qur’an, 2: 153).

Kumpenda Allah na kumtii kwa maamrisho Yake ndiyo msingi wa ibada na ndiyo lengo hasa la sisi wanadamu kuwepo hapa ulimwenguni.

Kwa ajili hiyo basi tunapojiuliza na kutafakari mafunzo tunayoyapata ndani ya Ramadhani na umuhimu wake kwa maisha yetu ya kila siku, inatubainikia kuwa lengo hasa la kuingia kwenye chuo hiki adhimu ni kuziweka nyoyo zetu ndani ya taqwa ya kumtii Allah kwa muda wote unaofuatia baada ya Ramadhani.

Allah anasema ndani ya Qur’an: “Enyi watu! Yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu, na poza kuponyesha yaliy- omo vifuani, na uwongofu, na rahma kwa Waumini. Sema, ‘Kwa fadhila ya Allah na rahmah Yake!’ Basi na wafurahi kwa hayo. Haya ni bora kuliko hayo wanay- oyakusanya,” (Qur’an, 9: 57–58).

Hivyo basi, ni wazi kabisa kuwa ibada ya funga ya Ramadhanini katika nguzo kubwa iliyo muhimu ya Dini ya Kiislamu iliyokusudiwa kutusaidia kama wa- nadamu katika kufanikisha lengo la kuwepo kwetu duniani kama Makhalifa wa Allah.

Kwa kuwa Ramadhani ni chuo adhimu cha kutuleta ndani yake taqwa pale tunapokuwa wastahamilivu na wanyenyekevu katika kufuata maamrisho ya Allah ndani ya nafsi zetu tunapata faida ya kuwa waadilifu na kuipigania njia ya Allah ndani ya nafsi zetu kwanza.

Vita hivi vya kuzilea nafsi kwa ajili ya Allah, huitwa jihad.

Jihad inakusanya mambo kuanzia vita dhidi ya wanaowapiga vita Waislamu, hadi vita dhidi ya yale yote yaliyokatazwa na Allah ili kupata daraja ya juu kabisa ya mafanikio katika maisha ya Mwislamu mbele ya Allah. Juu ya hili Allah anasema ka- tika Qur’an: “Wale walioamini, na wakahama, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Allah kwa mali yao na nafsi zao, hao wana cheo kikubwa zaidi mbele ya Allah. Na hao ndiyo wenye kufuzu,” (Qur’an, 9: 20). Wengi wetu huelewa neno ji- had ni kuchukua silaha na kwenda vitani tu. Jihadi kubwa haswa ni kupigana na nafsi zetu kwa kuacha yale yote tuliyokatazwa na Allah na Mtume wake na ku- fanya yale tuliyoamrishwa ndani ya Uislamu. Hili ndilo lililokuwa hasa lengo la swaumu yetu ya Mwezi wa Ramadhani.

Kichocheo

Swaumu yetu iwe ni kichocheo cha kusimama katika njia ya haki kwa kumtii Allah kwa kufuata maamrisho yake na kujiweka mbali na makatazo yake. Ikiwa tutafanya hivi tutafuzu mbele ya Allah kwa kuishi maisha bora hapa duniani na kutarajia mema kesho Akhera.

Ikiwa wahenga walinena Ku- vunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi, Hivyo basi kwisha kwa Ramadhani isiwe ndiyo mwisho wa sisi kufanya mema na kuishi nje ya mipaka ya Allah.

Bali tubebe tabia zote njema tulizojifunza ndani ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kwa kufanya hivyo tu, ndiyo tutakuwa Waislamu wa kweli. Aliyekuwa anaabudu Ramadhani basi Ramadhani imeshaaga, lakini aliyekuwa anamwabudu Allah, basi Allah Yu hai daima kama anavyosema:

“Allah, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Aliye hai daima, Msimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kufikia kuelewa chochote kuhusu ujuzi Wake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi vi- wili hivyo. Naye ni Mwenye Ul- uwa,Ametukuka, Adhimu; Mkuu kabisa,”

(Quran, 2: 255)